Here are the lyrics to the song “Amepotea” by Mbosso:
VERSE 1
Vipeperushi vinasambaa
Eti natafutwa nimepotea
Wiki imekata
Ndugu wamechachamaa
Wananitafuta mwezi umekataa
BRIDGE
Kazini sionekani
Yupo wapi huyu simuni
Sipatikani
Yupo wapi huyu
Baba kaniulizia
Yupo wapi huyu
Mama ahisi kulia
Yupo wapi huyu
CHORUS
Mimi nimezamaaa
Katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi
Nimezama katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi
VERSE 2
Siwe handiti pule mwanarajabu
Mliomkuta Tanga
Sijafanywa msukule
Msipate taabu
Kumaliza waganga
Amenirudisha shule
Hesabu maumbo kupanga
Penzi la wasasambule
Lenye protini vitamini na wanga
Ooh oooh ooooh
Ladha yake si sukari
Ni vichenza na malimau
Mechi zake huwa hatari
Ni chenga na mambao
BRIDGE
Kazini sionekani
Yupo wapi huyu simuni
Sipatikani
Yupo wapi huyu
Baba kaniulizia
Yupo wapi huyu
Mama ahisi kulia
Yupo wapi huyu
CHORUS
Mimi nimezamaaa
Katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi
Nimezama katika kina kirefu
Cha bahari ya mapenzi